Karibu WDEFI: Rasimisha Biashara Yako ya UWINGA!

Jiunge na mpango wa TRA unaokujali wewe Mfanyabiashara wa Mtandaoni. Pata LIPA NAMBA, Kitambulisho Rasmi, na uchangie maendeleo ya Taifa kwa urahisi na ada nafuu.

Anza Usajili Sasa!

Kuelewa WDEFI

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inatambua mchango mkubwa na ukuaji wa biashara zinazofanyika kupitia mitandao ya kijamii, maarufu kama "Uwinga". Mpango wa Kuwawezesha na Kurasimisha Winga Kidijitali (WDEFI) umebuniwa mahususi kwa ajili yenu – nyinyi mnaotumia WhatsApp, Instagram, TikTok, na Facebook kuendesha biashara zenu. Lengo letu ni kuwawezesha kurasimisha shughuli zenu kwa njia rahisi, kuwapa faida zinazoonekana, na kuwa sehemu rasmi ya uchumi wa kidijitali Tanzania.

Dira Yetu

Kuona uchumi wa kidijitali unaojumuisha kila mtu, ambapo "Winga" wanastawi na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya Taifa kupitia mfumo rasmi na wezeshi.

Lengo la TRA

Kupanua wigo wa walipakodi kwa njia endelevu, kukuza urasimishaji wa sekta isiyo rasmi, na kuboresha huduma kwa walipakodi kupitia teknolojia na ushirikiano.

Nafasi Yako Winga

Kwa kujiunga na WDEFI, unakuwa mfanyabiashara rasmi, unajenga heshima kwa wateja wako, na unashiriki moja kwa moja katika ujenzi wa Taifa kupitia mchango wako wa kodi.

Faida za Kujiunga na WDEFI

Kitambulisho Rasmi (WDEFI ID)

Pata namba ya kipekee ya WDEFI (mfano: 123456789-W01) inayotokana na TIN yako. Inakutambulisha rasmi kwa TRA na kuongeza uaminifu kwa wateja na wasambazaji.

Biashara Kidijitali

Fanya shughuli zako za kiuchumi kiganjani mwako bila wasiwasi ukiwa una tambulika na mamlaka ya mapato.

Kodi Nafuu

Changia kodi kwa ada moja tu ya mwaka (TZS 60,000), inayoweza kulipwa kwa awamu (robo mwaka, nusu mwaka, au mwaka mzima). Hakuna mahesabu magumu!

Mafunzo na Ukuaji wa Biashara

Pata mafunzo maalumu mtandaoni (kwa Kiswahili) kuhusu masoko ya kidijitali, huduma kwa wateja, usimamizi rahisi wa fedha, na uelewa wa kodi.

Utambulizi na Msaada

Fanya biashara kwa amani ukijua uko kwenye mfumo rasmi. Pata msaada na miongozo kutoka TRA unapohitaji.

Ushiriki Katika Ujenzi wa Taifa

Mchango wako mdogo wa kodi kupitia WDEFI unaenda moja kwa moja kwenye kuboresha huduma za jamii kama elimu, afya, na miundombinu.

Jinsi ya Kujiandikisha na WDEFI

Fomu ya Usajili

Jaza taarifa zako kwa uangalifu. Taarifa zote zimewekwa alama (*) ni lazima.

Ada na Malipo

WDEFI imebuniwa kuwa na ada nafuu na rahisi kwa wafanyabiashara wa Uwinga. Mfumo wetu wa malipo unazingatia ukuaji wa biashara yako na mapato unayotegemea kupata.

Kipindi Ada Inajumuisha
Mwaka Mzima TZS 60,000 Kitambulisho cha WDEFI, Mafunzo ya Kidijitali, Msaada wa TRA
Kila Nusu Mwaka TZS 30,000 Kitambulisho cha WDEFI, Mafunzo ya Kidijitali, Msaada wa TRA
Kila Robo Mwaka TZS 15,000 Kitambulisho cha WDEFI Mafunzo ya Kidijitali, Msaada wa TRA

Jinsi ya Kulipa Ada ya WDEFI

  1. Jiandikishe kwanza na upate Kitambulisho chako cha WDEFI
  2. Tumia simu yako kulipa kupitia njia zifuatazo:
    • M-Pesa: Lipa Bill GePG (Malipo ya Serikali)
    • Mixx by Yas: Lipa Bill GePG (Malipo ya Serikali)
    • Airtel Money: Lipa Bill GePG (Malipo ya Serikali)
    • HaloPesa: Lipa Bill GePG (Malipo ya Serikali)
    • ZanPesa: Lipa Bill GePG (Malipo ya Serikali)
  3. Weka Control Number yako ya WDEFI kwenye kumbukumbu ya malipo
  4. Subiri ujumbe mfupi wa uthibitisho kutoka TRA
  5. Pata risiti rasmi ya malipo na kitambulisho chako cha WDEFI kupitia barua pepe yako
Mobile Networks Mobile Networks
Tips TanQR TIPS TANQR
Airtel Money GePG

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Je, WDEFI ni nini hasa?

WDEFI (Winga Digital Empowerment and Formalization Initiative) ni mpango maalumu wa TRA ulioundwa kuwasaidia wafanyabiashara wa mtandaoni, maarufu kama "Winga", kurasimisha biashara zao bila ugumu. Mpango huu unakupa kitambulisho rasmi, na manufaa mengine kwa ada nafuu ya mwaka.

Ni nani anaweza kujiunga na WDEFI?

Mfanyabiashara yeyote anayeuza bidhaa au kutoa huduma kupitia mitandao ya kijamii kama WhatsApp, Instagram, Facebook, TikTok au Telegram anaweza kujiunga. Mpango huu umelenga hasa wafanyabiashara wadogo na wa kati wanaofanya biashara zao "uwingani".

Nitahitaji kulipa kodi kiasi gani?

Ada yako ni moja tu ya TZS 60,000 kwa mwaka, ambayo inaweza kulipwa kwa awamu (TZS 15,000 kila robo mwaka au TZS 30,000 kila nusu mwaka). Hii ndiyo kodi yako yote - hakuna malipo ya ziada au kodi nyingine utakazotozwa. Hii inafanya WDEFI kuwa rahisi na inayotabirika.

Nini tofauti kati ya TIN ya kawaida na WDEFI ID?

TIN ni Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi ambayo kila mlipakodi hupewa. WDEFI ID inatumia TIN yako iliyopo, lakini inakupa kitambulisho maalum cha WDEFI chenye muundo wa "123456789-W01". WDEFI ni mfumo rahisi zaidi ulioundwa mahususi kwa wafanyabiashara wa mtandaoni.

Je, nitapata mafunzo kuhusu biashara yangu?

Ndiyo! Wanachama wa WDEFI watapata mafunzo mtandaoni katika Kiswahili yanayolenga kuimarisha biashara zao. Mafunzo haya yatajumuisha masoko ya kidijitali, matangazo ya mtandaoni, huduma kwa wateja, usimamizi wa fedha, na msingi wa kodi. Mafunzo haya ni ya bure kama sehemu ya uanachama wako.

Nini kitatokea kama nisipojiunga na WDEFI?

WDEFI ni mpango wa hiari unaotoa faida za kurasimisha biashara yako. Bila kuwa mwanachama, unaweza kukosa fursa za kujenga uaminifu kwa wateja na kuwa sehemu ya mfumo rasmi wa kiuchumi. Lengo la TRA ni kukusaidia ukue, siyo kukuadhibu.

Je, WDEFI ni sawa kwa biashara kubwa?

WDEFI imeundwa mahususi kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati wanaofanya biashara mtandaoni. Ikiwa biashara yako imekuwa zaidi, ina wafanyakazi wengi, na mapato yako ya mwaka ni makubwa (zaidi ya TZS milioni 100), basi unaweza kuhitaji kufikiria njia nyingine za usajili wa biashara kupitia TRA na BRELA.

Maoni kutoka kwa Winga

Soma maelezo ya wafanyabiashara wenzako ambao tayari wamejiunga na WDEFI na jinsi mpango huu umewasaidia.

Nathan Christopher

"WDEFI imenisaidia kuwa na kitambulisho rasmi cha biashara yangu ya Instagram. Sasa wateja wananiamini zaidi na nimeweza kupanua soko langu."

Biashara ya Viatu Mtandaoni

Getrude Brighton

"Mafunzo ya WDEFI yamenisaidia kujifunza usimamizi bora wa fedha na kodi. Sasa nina ufahamu wa kutosha wa kusimamia biashara yangu kwa urahisi."

Biashara ya Nguo za Mtumba

Robert Mulla

WDEFI imenipa urahisi wa kuaminika na wafanya biashara ninapo chukua bidhaa zao. Hakuna tena wasiwasi wa kuacha dhamana kitambulisho cha WDEFI kinatosha."

Biashara ya Dawa za Asili

Wasiliana Nasi

Maelezo ya Mawasiliano

Ofisi Kuu

Sokoine Drive, Dar es Salaam

Simu

+255 XX XXX XXXX

Barua Pepe

services@tra.go.tz

Masaa ya Kazi

Jumatatu - Ijumaa: 08:00 - 17:00

Tufuatilie Mitandaoni

Tuma Ujumbe